KUENDELEZA BIASHARA KATIKA NYAKATI ZA MTIKISIKO WA UCHUMI.

Jeremiah Paul Wandili
4 min readMay 8, 2020
mtandao

Ikiwa ndio kwanza mwezi wa pili unaingia toka #covid-19 imeingia rasmi Tanzania. Umeshasikia mengi katika kujilinda na kuzuia ueneaji wa virusi vya corona. Pengine umeshasikia kuwa Biashara zitaathirika sana, na uchumi wa Dunia unayumba. Ndio biashara ya usafirishaji imeyumba sana hasa kwa ndege za Abiria, ukiachilia mbali za mizigo kwani sehemu kubwa biashara za kimataifa nazo zimepungua sana.

Kuhakikisha shughuli za biashara zinaendelea katika kipindi cha corona, makampuni mengi na biashara kubwa zimejiandalia mipango, mikakati, ili kupunguza gharama na kuokoa mtaji wa kuendeshea biashara. Mipango hiyo imelenga kuhakikisha Mauzo, kuangalia hali ya Usalama na uendeshaji wa biashara.

Je, wewe na biashara yako nini umekiona kikibadilika na unajipanga vipi kukabiliana na changamoto ya mtikisiko wa uchumi na uendeshaji wa Biashara. Hapa nimekuandalia hatua tano (5) za kuzingatia katika kupanga namna ya kuendelea na Biashara katika kipindi hiki cha #covid19.

#HATUA_YA_ KWANZA _ (1): Tathmini ya Athari katika Biashara.

Fanya thathmini ya athari katika uendeshaji wa biashara yako, katika kipindi hiki. Hatua hii inaangazia hali ya mapungufu katika biashara, uendeshaji katika kutoa huduma au uzalishaji wa bidhaa na usambazaji wake. Wakati wa kuandaa tathmini hii, ni vizuri ukaangalia madhara kwa wadau wako kama; Wafanyakazi; (Wafanyakazi ni nguzo muhimu sana katika biashara yako, hivyo lazima uangalie namna watabakia salama) Zingatia namna ya kufanya tathimini hasa ukizingatia sehemu kubwa yaweza kuwa wakifanyia kazi tokea nyumbani.

Tahadhali

Wateja; Ni muhimu kufanya tahmini kuona namna utaendelea kuwafikia wateja wako na kuwahudumia katika kipindi hiki ambacho yawezakuwa kuonana moja kwa moja ikawa changamoto. Wengine ni Wabia wako katika usambazaji/Wazabuni; Lazima kutathmini uwezo wa wazabuni wako, ili wasije kukukwamisha na kuangalia ni wazabuni gani ni muhimu au wanaulazima kubakia au kuendelea na kwa njia gani? Kwa mfano: wazabuni wa usambazaji chakula au usafi ofisini, kipindi hiki hakuna wafanyakazi ofisini, wanaweza kupunguzwa wakati ofisi mnaendesha mkiwa nyumbani. Kumbuka huu ndio wakati wa kuruhusu ubunifu na fikra tunduizi katika kufanya maamuzi.

#HATUA_YA_PILI_ (2): Andaa Modo (Model) Ya Mtazamo wa Biashara

Baada ya kukamilisha tathmini katika hatua ya kwanza. Hatua ya pili inakupa fursa kuangazia muondo wa biashara yako na namna utakavyo iendesha kwa kuzingatia mabadiliko ya uendeshaji, usimamizi na utendaji kwa kutazama mabadiliko ya Mkakati katika kuendesha biashara. Kwa mfano baada ya kuangalia namna utafanya kazi na wateja wako na wazabuni. Hatua hii inakupa nafasi ya kuonyesha Mpango Mkakati katika kuendesha biashara kwa mfumo mpya na ubunifu zaidi.

Zingatia mfumo wa usimamizi na ukusanyaji Fedha, uendeshaji, kwa kipindi cha meizi 3 hadi 6 lakini kila mwisho wa Wiki unaweza kurejea na kufanya tathmini katika utekelzaji wa mpango mkakati wa kuendeleza Biashara. Zipo njia nyingi za kuendesha na kusimamia biashara. Kumbuka kuwasiliana na wataalamu zaidi katika kufikia aina ya modo ya uendeshaji utakayo itumia.

#HATUA_YA_TATU_ (3): FANYA TATHMINI YA ATHARI NA ANDAA MPANGO KAZI.

Katika hatua hii itakuwezesha kufanya tathmini ya athari zinazoweza kujitokeza katika hatua ya 2 na kubainisha athari au hatari zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa modo yako ya uendeshaji na usimamizi wa Biashara. Kumbuka kuzingatia maeneo hatarishi kama Usimamizi wa Fedha, Rasilimali Watu, na za nje kama hali ya usambazaji wa huduma na bidhaa. Nyenzo za kufanyia tathimini zipo, kwa ushauri Zaidi wasiliana nami.

#HATUA_YA_NNE_ (4): ANDAA TIMU YA TAASISI YA KUKABILIANA NA KUHIMILI MAJANGA.

Kumbuka majanga hayana muda maalamu, hivyo ni jambo la dharula. Hakikisha unaandaa timu ya wataalamu watakao saidia kuendesha taasisi katika kipindi cha majanga na kuhakikisha shughuli za msingi za Taasisi haziathiriwi kwa namna moja au nyingine. Zingatia Afya ya Wafanyakazi, Wateja na wadau wengine, kwa kuhimiza mbinu mbalimbali zilizoshauriwa za kujikinga.

Kuporomoka uchumi

Hatua hii itakuwa ya manufaa makubwa kama utaandaa na mfumo wa mawasiliano na kuelimisha umma na wadau wako kwa ujumla. Katika utekelezaji wa itifaki ya mawasiliano katika nyakati ya Majanga, weka nyenzo na miongozo wazi kwa wafanyakazi, wateja na wazabuni ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa hatua ambazo uongozi wa kampuni umezingatia kwa ajili ya kudumisha na kuhimarisha usalama.

#HATUA_YA_TANO_ (5): MPANGO KAZI NA UFUATILIAJI

Katika kipindi cha majanga kama hili la corona, ni vizuri kujiwekea mpango wa kuhakikisha uendelezaji wa Biashara. Mpango madhubuti ni ule ambao unazingatia kuandaa viashiria ya kupima utekelezaji wa mpango. Hakikisha unafanya ufuatiliaji katika kupima hali ya Kifedha ya Taasisi au biashara na zingatia namna utakavyopima mkakati wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa kuzingatia uhimilivu wa biashara. Hakikisha ufuatiliaji wa Mpango unafanyika kila siku au kila wiki, ili kuleta ufanisi na kuangalia mabadiliko yanayoweza kuleta athari katika uendeshaji, usimamizi wa Biashara.

Hakikisha unapata Takwimu na taarifa sahihi ambazo zitasaidia kufanya maamuzi sahihi katika kuendeleza biashara huku ukiepuka hasara inayoweza kujitokeza kwa mara moja. Katika kipindi cha janga kama hili, mambo mbalimbali yanatakiwa kuzingatiwa na kuhuisha mpango wa uendelezaji wa Biashara kwa kuzingatia mabadiliko ya ghafla. Kama nilivyokwisha sema, hali ya uwepo wa fedha za uendeshaji ni muhimu sana, hivyo zingatia usimamizi wake bila kupoteza mtaji wa uendelezaji Biashara.

Kumbuka, walinde wafanyakazi ambao ni muhimu sana katika kutoa huduma au kuzalisha bidhaa, linda Afya ya Akili, walinde dhidi ya virusi vya corona kwa kufanya kazi kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya na mashirika ya Afya Duniani. Ndio kumbuka kuwalinda na wateja pia…. Ugonjwa huu unapunguza hata idadi ya wateja wako, hivyo tumia muda kuwasaidia wateja kujikinga.

#Biashara #Mtaji #Mpangomkakati #KuendelezaBiashara

--

--

Jeremiah Paul Wandili

| Community Development | BDSPM Consultant| YALI Alumni, Founder & Executive Director @woteinitiative Youth Leadership Advisory Board, Member #YLAB @DOTTanzania