Mbinu 5 za Kumiliki Soko.

Jeremiah Paul Wandili
5 min readJun 5, 2020

Biashara yoyote ile inategemea fedha kuendesha shughuli zake, na fedha zinatokana na kuuza bidhaa au kutoa huduma. Biashara ambayo haitengenezi fedha ufikia ukomo na hatimaye kufa. Na fedha utokana na mauzo ya bidhaa ambazo wateja wanakuwa wamefanya uamuzi wa kununua bidhaa au kulipia huduma.

Data Masoko

Baada ya kuwasiliana na wajasiriamali na wafanya biashara wengi ndani ya Afrika ya Mashariki nimegundua kuna “DILEMA” kubwa kwa biashara kama mfumo na wafanyabiashara ambao ni wamiliki wa biashara. Ni kama wana ahadi kuwa hali ya sasa itabadilika, ila wamebakia wakisubiri bila ya kujiandaa kukabiliana na MABADILIKO.

Kwa wataalamu wa mambo ya kijamii hali hii inatafsiri mabadiliko makubwa katika mfumo mzima wa kukuza biashara, kupanua masoko na kuongeza mauzo. Hivyo mabadiliko ni lazima kuchukuliwa kwa mtazamo chanya ili kuandaa mkakati wa kukabiliana nayo.

Ukitazama nadharia ya mabadiliko ya biashara na mpango wa Masoko, utagundua hata kabla ya janga la #Covid-19 tayari kulikuwa na mabadiliko ya taratibu katika mfumo mzima wa uendeshaji biashara. Lakini kupitia janga hili mabadiliko hayo yamefanyika na yanaendelea kufanyika kwa haraka sana na yanaleta matokeo tofauti kwa wengi.

Leo ninakushirikisha mbinu 5, ili uweze kuokoa Bishara yako na kutimiza malengo yako. Mwaka 2020 tayari ni mwaka ambao umeshaingia katika historia kubwa ya kuvuruga hali ya uchumi, kijamii na pia mabadiliko ya Tabia. Hivyo imeathiri namna biashara zilivyokuwa zinafanyika, umepelekea kushuka kwa soko na nguvu ya wateja kununua.

Mwenendo wa mwaka 2020 umenikumbusha nikushirikishe Mbinu 5 muhimu ambazo utazitumia kujimilikisha soko lako. Kumbuka wateja wazuri na wakudumu ni haki yako.Lakini ni lazima ufanye kazi ya ziada ili kubakia katika ushindani. Fuatilia Mbinu 5 kwa umakini, endapo utakuwa na swali tuma kwa barua pepe; datamasoko@gmail.com au piga namba +255655147271

#1. Wekeza katika mawasiliano.

Katika mbinu bora zilizothibitishwa za kukuza biashara ni mawasiliano. Katika janga hili la Covid-19 kila mmoja yupo katika taharuki na wengi wamejawa na hofu. Tumia mfumo wako wa mawasiliano kuwajengea Imani wateja wako, kuwafariji na kuwahamasisha kuchagua mabadiliko chanya na kuacha kulalamika. Wakati wengine wapo kimya na katika hali ya hofu kuhusu kuanguka kwa uchumi.

Wewe endeleza mawasiliano chanya na wateja na kujua mahitaji yao zaidi, jitahidi kuwafuatilia kujua wanaendeleaje, wengine wamefiwa, wengine wamekufa; Biashara yako inafanya nini? Wekeza katika kujenga mahusiano na shiriki katika matatizo yao. Hii itasaidia kuona hausubiri tu wakati wa furaha na kwamba unajali wateja wako hata nyakati za shida.

#2. Endelea kutangaza ofa na punguzo la bei

Usiache, wala usisahau kuwatangazia wateja wako wa zamani na hata wapya kuhusu OFA na punguzo la Bei. Wafanya biashara wengi wanasubiri msimu wa Sikukuu ambapo kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa au huduma kutoa ofa na kutangaza punguzo. Nakwambia huu ndio wakati mzuri wa kutangaza Ofa na kutoa punguzo ili kuwajali wateja wako na watarajiwa wako katika soko.

Endelea kutangaza ofa, endela kutangaza punguzo….. Maana hali ya uchumi imebana sana, hivyo na wateja wako wanatamani kupata bidhaa na huduma zako kwa unafuu. Usipofanya hivyo watachagua bei pasipo kujali ubora na hatimaye watachagua kuama pole pole na kwa hakika utapoteza wateja.

#3. Endelea kufanya utafiti wa mabadiliko na mahitaji ya Soko

Katika nyakati hizi zinazobadilika kwa kasi sana, tabia, mfumo wa maisha, teknolojia na vizazi (Generation) Zaidi ya yote uwezo wa wateja kununua. Wafanya biashara wanahitajika kufanya tafiti mara kwa mara ili kujua mahitaji, hali na uwezo wa wateja. Katika kipindi hiki cha janga la #Covid-19 ni muhimu sana kwa Biashara kutambua mahitaji ya muhimu kwa wateja ili kusaidia na kutafuta njia bora na rahisi inayoweza kutumika kuwafikishia huduma na bidhaa.

#4. Kuwa Karibu na Wateja wako.

Kuna njia nyingi za kuwafikia wateja wako, baada ya kuwa umefanya utafiti utagundua njia bora na rahisi za kuwafikia wateja wako. Moja ya jambo muhimu sana katika kukuza biashara na kujenga BRAND, ni kutangaza. Hapa kuna njia rahisi kwa kutumia mitandao ya kijamii. Tumia mbinu ya kutangaza kupitia mitandao ya kijamii. Kwa ushauri wa njia bora za kutumia mitandao ya Kijamii, fuatilia ukrasa huu wa Instagram kuna mbinu zimeandaliwa kukusaidia kutumia mitandao ya kijamii kutangaza na kuwa karibu na wateja wako. Njia nyingine anza kwa tumia mtandao wako kutangaza huduma, ofa na punguzo la bei kwa wateja na watarajiwa wa wateja wako. Usichoke kutangaza. Be social. Jenga biashara yako.

#5. Tengeneza kiota chako (Niche)

Moja ya mbinu nzuri sana ni hii ya kutengeneza kiota. Wakati wa kutengeneza kiota chako, tumia taarifa mbalimbali zilizokusanywa wakati wa utafiti. Chagua eneo na aina ya wateja utakao wamudu. Tumia eneo dogo kutengeneza kiota kabla haujapanua eneo la kiota chako, hii itakusaidia wale wateja wanaopenda na kuthamini bidhaa zako na huduma zako watawashirikisha wengine, hivyo utapata mrejesho mzuri katika kukuza na kuendeleza biashara yako.

Kumbuka wateja wengi wanajenga uaminifu kutokana na huduma unazotoa na bidhaa unazowauzia..usisite kuomba mrejesho na usiogope kupokea lawama. Jitahidi kupokea maoni na ushauri. Hii inasaidia wateja kumiliki biashara na kuamua kukusaidia kuikuza na kwa uaminifu wao, wanaendelea kuitangaza na kuwashauri wengine katika mtandao wao kuamini katika huduma na bidhaa zako.

Ikiwa umeanzisha Biashara ya kuuza bidhaa au kutoa huduma jiunge na ukrasa wa Data Masoko Twitter, Instagram na Facebook pia Subscribe katika Idhaa (Channel) ya Youtube ya Data Masoko. Kuna program kubwa zinakuja kwaajili yako. Data Masoko ni wabobezi katika maswala ya Kujenga Masoko ya Kidigital na zaidi kukuza BRAND. Data Masoko ni “Uhakika Sokoni”.

Ahsante kwa kuchagua kuisoma makala hii, na kuchagua kufuatilia na kufanyia kazi ushauri wa bure… Kumbuka USHAURI Bure, Gharama Utekelezaji. Data Masoko “Uhakika Sokoni”.

Makala hii imefadhiliwa na Data Masoko, endelea kujiunga nami kila siku ya Ijumaa hapa hapa nikikuletea dondoo za kukusaidia kukuza na kuendeleza Biashara yako. Ahsante sana.

--

--

Jeremiah Paul Wandili

| Community Development | BDSPM Consultant| YALI Alumni, Founder & Executive Director @woteinitiative Youth Leadership Advisory Board, Member #YLAB @DOTTanzania